SALAMU NA SHUKRANI
Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa kila mmoja wenu aliyetufariji katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kumpoteza mke wangu mpendwa Patrizia (Rah'ma), Mama Amani.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, kwa upendo, muda wenu na kujitoa kwenu kuhakikisha tunamsitiri mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu awazidishie pale mlipotoa michango yenu ya hali na mali kupitia Shirikisho la Watanzania na Jumuiya zote mlizoshiriki.
Hatuna cha kuwalipa zaidi ya shukrani.
Mola awape thawabu na baraka tele nyinyi na familia zenu, siku zote.
Amina.
Fabrah ( Fab-Moses) Shinanjee
Husband
Naomba nafasi kuwashukuru nduguzangu wote kwa kua pamoja nami kwenye msiba wa mwanangu , michangoyenu na mloojaaliwa kunipigia simu, Asanteni sana, Mungu atubariki sote tuendelee Kushikamana na Kuimarisha Udugu wetu, bless you all!
Father
Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
Napenda kuwashukuru kwa dhati wanashirikisho kwa mchango wenu wa £8, 830 katika mazishi ya mama yetu Khadija Sollo Kilumanga. Upendo na msaada wenu umeonyesha jinsi gani tunaweza kuungana na kuwa kitu kimoja wakati wa kipindi hichi kigumu. Asante kwa miyoyo yenu ya ukarimu na kwa kuwa pamoja nasi katika kutuwezesha kumsafirisha na kumzika mama yetu salamaTanzania. Mungu awabariki nyote kwa ukarimu wenu na upendo mlioonyesha. Tuzidi kumuomba Mungu ailaze roho yake mahali pema. Amin.
Mariam Kilumanga
Daughter
Asalam Aleykum ndugu zangu wa shirikisho mimi Faiza Diriye natoa shukran zangu za dhati kwa kutufariji mimi na familia yangu katika msiba mkubwa uliotupata. Nashukuru wana shirikisho wenzangu kwa moyo wenu wa ukarimu kwa kutuchangia kwa hali Mali. Sina cha kuwalipa ila Mwenyezimungu Mwingi wa Rehema atawalipa pale mlipopunguza.
Wife
SHUKURANI
Watoto na Familia ya Ms Delina Maro tunapenda kutoa taarifa kwa Shirikisho la Watanzania UK kwamba mazishi ya Ms Delina Maro, mama/ndugu yetu yalifanyika juzi tarehe 18/6/24 katika makaburi ya Enfield Lawn Cemetery, North London.
Tumefarijika sana kwa michango ya fedha, shada la maua na wanashirikisho walioweza kujumika na sisi katika mazishi.
Hatuna jinsi ya kuwalipa bali tunaomba Mwenyezi Mungu awabariki. Na pia tunaomba shirikisho hili liendelee kuimarika na kusaidia jamii yetu hapa UK.
Asanteni sana.
Bwana ametoa na Bwana Ametwaa. Jina lake lihimidiwe milele. Amina
Daughter
Habari zenu ndugu zangu. Ni matumaini yangu kuwa nyote muwazima wa afya . Kwa niaba ya familia ya ndugu yetu marehemu Medina natoa shukurani zetu za dhati kwa michango yenu ya Hali na Mali🙏🏽 katika kufanikisha mazishi ya dada yetu/mama yetu na ndugu yetu.
Mwenye ez mungu awabariki na awaongezee pale mlipopunguza ktk kufanikisha shughuli hii .
Ahsanteni Sana na m-barikiwe Sana
Relative
Kwa niaba ya Familia ningependa kutoa shukrani za dhati kwa wanajumuiya ya shirkisho kufuatia Msiba wa Mama, Dada, Ndugu yetu UMMI MUSTAFA.
Wanajumuiya mmekuwa msaada mkubwa sana kuanzia marehemu alipokua anaugua U.K na baadae Tanzania, wakati wa Mazishi, na sasa kwa mchango huu.
Bila hata kufahamu malengo ya jumiuya hii hapo mwanzo, Faraja , upendo na msaada wa hali na mali mliouonesha kwa mama yangu tangu anaugua hadi sasa, umetuonesha taswira ya jumuiya hii.
Kibinaadam hatuna cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kuwazidishia na kudumisha muunganiko huu.
Kwa Uongozi Kaka Tito, Dada Halima na wengine wote mwenyezi mungu aendelee kuwapa busara ya kuongoza na tunashulikuru sana
Uncle
Tumepokea Jumla £9,500.
Kwa niaba ya familiya yetu natoa shukraan zetu za dhati kwa michango yenu na ukarimu wenu, kuweza kusimama na sisi kwa hali na mali ktk kipindi chote cha majonzi ya kuondokewa na mama yetu mpenzi. Na pia tunawashukuru viongozi woote wa shirikisho kwa kulisimamia jambo letu kwa upendo na juhudi zenu za kujitolea ktk kuimarisha umoja wetu. Allah awalipe mazuri.
Hakika ALLAH ni Karim, humgawia rizki amtakaye na bila ya hesabu. Kwa hili tunawaombea wanashirikisho woote, Mola awazidishiye kwa kile ambacho mlichopunguza kwenu na awalipe kheri zaidi, Ameen.
Shukraan.
Daughter