• Faridah
  • 04/10/2025 15:17:35
  • 3 Comment(s)

Kuhusu Website na Maujanja ya Michango

Wanachama wa Shirikisho
Nitaendelea kuwapambania na kuwafungua macho, wanachama wenzangu.
Mtakumbuka kuwa kufungwa kwa magroup yetu ni hila iliyokusudiwa kutunyamazisha milele. Hakuna siku au tukio lolote muhimu litakalotupa nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yetu kama wanachama, kwa sababu Shirikisho linaendeshwa kwa maslahi binafsi ya Bwana na Bibi IT na Machawa.
Baada ya tangazo la Tito nimekutana na Mkataba wa Mkandarasi wa mtengenezaji wa tovuti (Web Developer), ambao unadaiwa kuruhusu wanachama kutoa maoni kupitia website. Hata hivyo, mkataba huo umechakachuliwa kwa zaidi ya mwezi mzima; jitihada zote zinaonekana kuelekezwa katika kuwanufaisha wachache na kuwaibia wanachama. Ninawasihi msikubali kudanganywa wala kuburuzwa.
Tovuti yenyewe iko mikononi mwa Bwana na Bibi IT, ambao wana uwezo wa kuandika na kufuta chochote wanachotaka. Hivyo basi, hakuna maana yoyote kuandika maoni humo kwani yatafutwa tu.

Leave a Comment

You must be a Shirikisho member to reply to messages or to react to comments

Login Become a Member
3 Comment(s)
Faridah

Wanachama wa Shirikisho.
Nitaendelea kuwapambania na kuwafungua macho, wanachama wenzangu.
Mtakumbuka kuwa kufungwa kwa magroup yetu ni hila iliyokusudiwa kutunyamazisha milele. Hakuna siku au tukio lolote muhimu litakalotupa nafasi ya kuzungumza na kutoa maoni yetu kama wanachama, kwa sababu Shirikisho linaendeshwa kwa maslahi binafsi ya Bwana na Bibi IT na Machawa.
Baada ya tangazo la Tito nimekutana na Mkataba wa Mkandarasi wa mtengenezaji wa tovuti (Web Developer), ambao unadaiwa kuruhusu wanachama kutoa maoni kupitia website. Hata hivyo, mkataba huo umechakachuliwa kwa zaidi ya mwezi mzima; jitihada zote zinaonekana kuelekezwa katika kuwanufaisha wachache na kuwaibia wanachama. Ninawasihi msikubali kudanganywa wala kuburuzwa.
Tovuti yenyewe iko mikononi mwa Bwana na Bibi IT, ambao wana uwezo wa kuandika na kufuta chochote wanachotaka. Hivyo basi, hakuna maana yoyote kuandika maoni humo kwani yatafutwa tu.
Kama kweli Shirikisho ni mali ya wanachama, basi wanachama wanapaswa kupewa heshima ya kusema, kujadili, na hata kukosoa kupitia magroup yao. Kwa nini magroup yamefungwa? Kwa nini sauti za wanachama zinanyamazishwa?
Ni wakati wa kuachana na utawala wa kiimla na upigaji unaoandaliwa kupitia mkataba huu kandamizi. Hakuna katiba yoyote inayosema mwanachama lazima achangie zaidi ya rambirambi pekee, ambayo kiasi chake ni £3.50 , si zaidi ya hapo. Hivyo basi, kwa nini tunalazimishwa kuchanga zaidi bila mkataba rasmi na bila nafasi ya kujadili kwenye magroup?
Je, rasimu ya Katiba nayo itachezewa vivyo hivyo, kwa kuwanyima wanachama haki ya kushiriki na kutoa maoni juu ya vipengele vyake? Ni lini Tito tuliyempa Uratibu wa Muda tu ataona umuhimu wa kufungua magroup ili wanachama wawe na haki ya kutoa maoni yao kwa uhuru?
Tovuti yenyewe imejaa changamoto. Mpaka leo, malipo ya baadhi ya wanachama yamepotea na wanaonekana hawajachanga, ilhali walichanga. Tarehe za kujiunga zimebadilishwa kiholela, na malipo mengine yameandikwa kama late payments. Wengi wanahangaika kila mara msiba unapotokea wakijaribu ku-upload risiti zao bila mafanikio.
Kwa nini basi wanachama wanalazimishwa kutoa maoni kwenye tovuti hiyo? Hakuna mwanachama hata mmoja aliyewahi kutoa maoni yake humo, zaidi ya Bwana na Bibi IT wanaojisifu kana kwamba Shirikisho ni mali yao, ilhali ni wanachama ndio wanaochangia kila kitu.
Masharti magumu na bei kubwa walizoweka zimelenga kulifanya Shirikisho lisiwe na uwezo wa kumtafuta mkandarasi mwingine. Hayo hayakuwa makubaliano yetu. Hii ndiyo sababu nilizuiwa kuingia kwenye mkutano , walijua wazi kuwa ningeanika njama zao za wizi. Eti faini ya £ 5000 kwa Shirikisho, mitano tena kwa Developer 😂
Mimi, Faridah Gullam, nitaendelea kuwa msema kweli na mtetezi wa wanachama wa Shirikisho. Tusikubali kuchangishwa bila mkataba ulio wazi na bila nafasi ya kujadili kupitia magroup yetu. Hiyo ni pamoja na rasimu ya Katiba, ambayo lazima itolewe kwa majadiliano ya wazi.
Tukatae kuburuzwa, tukatae udanganyifu, na tudai haki yetu kama wanachama halali wa Shirikisho.
Msema kweli daima na mtetezi wa wanachama wa Shirikisho
Faridah Gullam

BBC1

Tovuti yenyewe imejaa changamoto. Mpaka leo, malipo ya baadhi ya wanachama yamepotea na wanaonekana hawajachanga, ilhali walichanga. Tarehe za kujiunga zimebadilishwa kiholela, na malipo mengine yameandikwa kama late payments. Wengi wanahangaika kila mara msiba unapotokea wakijaribu ku-upload risiti zao bila mafanikio.

Dada Faridah , Nimesoma malalamiko yako uliyotoa zidi ya kitengo cha IT. Noamba niikuhakikishie tuhuma hizo si za kweli kabisa na kama una ushahidi nakuomba uwasiliane na mimi au unitumie. namba zao asap niwasiliane nao hili niwasikie changamoto zao. Misiba ya hivi karibuni nimekuwa. nikipokea wastani wa simu 10 maximum . Matatizo mengi nimejaribu kuya solve pamoja na Team yetu nzima . Nilitoa tangazo kwenye platform zote kuwa wenye shida yoyote kwenye portal wanitafute ni wachache waliojitokeza . Ninaomba unitumie ushahidi wa malipo ya wanachama yaliyopotea kama ulivyodai kwenye message yako na namba zao za uanachama.

Tovuti ni mali ya wanachama wote na siyo viongozi kama unavyodai wewe.

Swala la mkataba wa Developer lipo salama chini ya. viongozi wa wawakilishi wetu sidhani kama wataweza kuburuzwa viongozi wenu wapo Imara sana.
Kufungwa kwa magroup ya whatspp tulipiga kura wote na decision ikatolewa na wanachama na hatuwezi kwenda kinyume na matakwa yenu.
Ningekushauri kama wewe ni mwanachhama hai wa shirikisho basi tuma complainning zako wa
info@shirikisho.org utajibiwe duku duku zote .

Dr P

1. Dada yangu, wewe sema unajipambania nafsi yako, maana shirikisho ni hiari na kila mtu hapa unajiwakilisha mwenyewe kwenye ili kundi la kufa na kuzikana. Hii iko straight forward, active member akitangulia mbele ya haki, unamwekea next of kin wake £3.5 ndani ya siku 7 na kuweka kidhibitisho chako, as simple as that!

2. Wanashirikisho tuli vote majority rukhusa ya platforms za WhatsApp kufungwa na kutumika only kwa ajiri ya matangazo ya misiba au yale ya muhimu tu. Labda ungelezea unachotaka kujadili ktk kufa na kuzikana?
Hata hivyo kuna email, namba za simu nadhani zaidi ya 3, platform ya telegram, website, ambavyo viko wazi 24/7 kuuliza chochote kama mtu ana shida na kutoa maoni.

3. Sijui uelewa mdogo au haya ni makusudi? Misiba 22 imechangiwa! Ina maana haujui kuwa wewe, mimi na wote tunalipa moja kwa moja account za wafiwa! Na kwamba kabla msiba haujatangazwa unakikiwa na wawakilishi? Sasa huo upigaji unatokea lini na wapi? Na kama basi unayo taarifa, Lete vielelezo vya upigaji au hata mifamo ya hayo maslahi binafsi ulosema ili wote tuyatambue.

4. Changamoto za Tovuti...... Kumbuka kutofautisha tatizo la mtumiaji (user error), maana hilo siyo tatizo la Tofuti. Licha ya hilo, zipo video na miongozo kadhaa jinsi ya kutumia tovuti hatua kwa hatu, pia namba za simu kuuliza au kuelekezwa, n.k. Na kuna wasiojiweza, wanasaidiwa kila msiba! Kwahiyo karibu utoe mawazo, pendekezo ya nini unadhani kifanyike zaidi ya utaratibu wa sasa, maana hiyo ndo itasaidia zaidi kuliko hizi bla bla.

5. Wanachama kulipia tovuti.... Mahamuzi yanapitishwa na wawakilishi, lakini pia hata wewe , kama ni active member, basi saidia kutafuta/ lete au toa mwongozo wa Developer unayemjua atakayetutengenezea na kurusha tovuti bure, au kwa bei pungufu kuliko ya sasa, hadi kufikia hatua ya kikazi (system functions) ilikofikia portal! Nina uhakika kila mwanachama hai angependa kusikia hiyo habari njema na endelevu.

6. Wanachama wote hapa ugenini tuna shughuli zetu mablimbali za maisha na tunazifanya mida na wakati tofauti, so, maoni yakitolewa ktk website, yatakuwa wazi na kuwepo 24/7, hivyo kila mtu anapata nafasi ya kuyapitia kwa wakati wake, hii ni more of a practical issue ukilinganisha na njia zingine mbadala ambazo zilitumika hapo awali.

7. Ungetueleza 1, 2, 3 ambazo wewe unaona members tunaburuzwa au kudanganywa au kuibiwa? Weka mifano wazi ili sote tupate kufahamu.

Kwa ufupi, Dada yetu kama wewe ni mwanachama hai, basi shirikisho ni letu sote, na lengo lake ni kufa na kuzikana tu. Toa mawazo endelevu badala ya kushutumu na kuleta mihemuko ya kupotosha! Kama kuna sehemu unaona mapungufu au maboresho, yaweke bayana badala ya kejeli za sijui IT wanaiba, wana agenda za siri, Tito kafanya hiki, members tunaburuzwa, n.k. Na kama una issues na watu binafsi, basi malizaneni nao huko nje kwa nje.

Karibu, leta hoja endeleve badala ya gossips, ili kwa pamoja tulisogeze gurudumu la Shirikisho wakati huo tukisubiria zamu yetu ya Kihama😔🙏.